Monday, 7 November 2016
AZAM FC YAPATA PIGO, YAPOTEZA KIONGOZI WAKE
The Author
DK.SHEIN: ICC HAWANA UWEZO WA KUTUSHTAKI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein amesema Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), haina uwezo wa kuhoji uchaguzi wa visiwa hivyo.
Aliwataka wananchi wa Kisiwa cha Pemba kupuuza taarifa kwamba kuna Serikali nyingine itaingia madarakani visiwni humo, badala yake waendelee kufanya kazi kwa bidii kwa kushirikiana na SMZ.
Taarifa ya Ikulu ya Zanzibar iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari ilisema Dk. Shein amewaambia wananchi kisiwani humo kwamba Serikali anayoiongoza iko madarakani kwa mujibu wa Katiba na inaendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM hadi mwaka 2020.
“Wanaisingizia ICC, wanadanganya tu haina uwezo huo wa kuhoji uchaguzi wa Zanzibar ulioendeshwa kwa mujibu wa Katiba yake,” alisema Dk. Shein ambaye yuko kisiwani Pemba kwa ziara ya kikazi.
Dk Shein alionyesha kukerwa na uzushi huo. Aliwakumbusha wanasiasa wanaoeneza uvumi wa kuingia madarakani kwa Serikali nyingine akisema kiongozi anayetaka ushindi ni lazima ashiriki uchaguzi, achaguliwe na wananchi na atangazwe na Tume ya Uchaguzi kuwa ni mshindi.
“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo na mimi ndie Rais. Ni serikali halali kwa mujibu wa Katiba ya mwaka 1984,” alisema.
Aliwahakikishia wananchi hao kwamba hakuna nchi wala taasisi ya ndani au ya nje inayoweza kuiondoa Serikali iliyopo sasa, wala hakuna wa kuhoji uhalali na uwepo wake.
“Hakuna nchi inayoapisha Rais mara mbili, mimi sina wasiwasi na Serikali yenu haina wasiwasi na tuko hapa kuwatumikia ili kuendeleza nchi yetu, maneno haya yanawapotezea muda wenu tu,” alisema na kufafanua:
“Serikali hii ni ya wananchi waliyoichagua na wasioichagua, waliopiga kura na wasiopiga kura. Wapo wanayoitaka na wasiyoitaka, wote hao wanafanya kwa hiari yao, lakini mwisho wa yote kwa kuwa tayari imewekwa madarakani na wananchi wenyewe kupitia uchaguzi ulioendeshwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar hawana budi kuitii.”
KUWA KARIBU NAS
The Author
KIFO CHA SITTA CHAACHA SINTOFAHAMU BUNGENI
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu amekumbana na kibano cha wabunge baada ya wawakilishi hao wa wananchi kuzua zogo wakilazimisha shughuli za kikao cha sita ziahirishwe kuenzi kifo cha Spika mstaafu, Samuel Sitta.
Sitta aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tisa na pia Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, alifariki dunia nchini Ujerumani.
Tafrani hiyo imeanza baada ya kuwatambulisha wageni waliofika bungeni ambapo Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Munde Tambwe alisimama na kuomba mwongozo kwa Spika.
Amesema kutokana na taarifa za msiba wa Sitta, Taifa na hususani wakazi wa Tabora wamepoteza kiongozi mahiri.
“Sitta alikuwa mbunge wa muda mrefu alikuwa Spika wa Bungekwa muda mrefu na pia alikuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba la Kihistoria,” amesema akimwaga machozi huku akikatiza mazungumzo.
“Kwa niaba ya wabunge wenzangu, naomba Bunge liahirishwe ili kupata muda wa kuomboleza na kutafakari,” amesema.
Ombo hilo liliungwa mkono na Mbunge wa Manyoni Magharibi (CCM), Elibariki Kingu kwa kumfuata Munde kwenye kiti chake na kumbembeleza.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu, amesema licha ya kwamba anakubaliana na mbunge huyo kuwa msiba ni mkubwa na umeligusa Taifa na kwamba ofisi ya Bunge ilimhudumia kwa matibabu, Bunge linaendeshwa kwa kanuni.
“Kanuni zinasema anapofariki mbunge. Mheshimiwa Spika alishastaafu kuwa mbunge, naomba tuendelee hadi hapo kutakapokuwa na maelekezo mengine,” amesema Zungu.
Kauli ya Zungu ilimnyanyua Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kwa kutumia Kanuni ya Bunge ya 152 ambayo aliinukuu, “Endapo mbunge atafariki wakati bunge likiwa katika shughuli zake, Spika ataahirisha shughuli za Bunge kwa siku hiyo kwa ajili ya kuomboleza.
“Toka nchi yetu ipate uhuru tulikuwa na maspika kadhaa, maspika wote waliopoteza maisha baada ya kustaafu, Bunge halikuwa kwenye vikao vyake.
The Author
UKWELI KUHUSU UGONJWA WA TEZI DUME
TEZI DUMEMojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ndoa. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen), aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike.
The Author
CUF; BODI YA UDHAMINI

The Author
MWANAUME UWE NA MSIMAMO KAMA HUU
*MAMA MKWE* 👂🏾
_Ilikuwa wakati wa mchana ambapo mume alirejea nyumbani akiwa na habari mbaya._
*MUME:* _Mpenzi, nimepigiwa simu: Mama hajisikii vizuri. Tunaweza kwenda kumnunulia baadhi ya mahitaji kwa ajili ya kumtembelea?_
```Tafadhali andika orodha ya mahitaji kisha tuondoke.```

*MKE:* _Orodha ya vitu hivyo sio muhimu, tutanunua tu kabichi 2 na lita 2 za mafuta ya kupikia._
*MUME:* _Vitatosha kweli?_
*MKE:* _Ndiyo mpenzi, hakuna haja ya kupoteza pesa, vitatosha._
```Walielekea mjini na kununua kabichi 2 na lita 2 za mafuta ya kupikia. Wakati wakinunua mume alimuuliza mkewe tena kama vitu hivyo vingetosha.```
```Walianza safari kuelekea kijijini, na walipofika kwenye eneo la njia panda yenye barabara zinazoelekea vijiji mbalimbali, mume alikata kona kuelekea kwao na mke.```
*MKE:* _(Kwa mshituko) tunaelekea wapi mpenzi? Nilidhani tunaenda kumtembelea mama yako._
*MUME:* _Ndiyo, ndiko tunakuelekea. Ni mama yako (mama yetu) ndiye anayeumwa._
*MKE:* _(kwa mshituko na kilio), lakini mahitaji haya hayatoshi. Turudi tuongeze vitu vingine._
*MUME:* _Hapana! Nilikuuliza tena na tena kama mahitaji hayo yanatosha, ukaniambia “NDIYO”. Hakuna kurudi….._
```FUNZO:```
```Wafanyie wenzako kile unachotaka ufanyiwe!!```
*Yes, hatupendagi ubaguzi sisi.*
🙈🙈🙈‼
The Author
Featured
-
AyoTV
Diamond kuhusu ushindi wa Rayvanny BET 2017
Mwimbaji staa wa Bongofleva, makofi mengi amepigiwa kwenye utunzi wake pamoja na ukali wake wa melody, anaitwa Rayvanny kutoka...
-
AyoTV
Okwi amerudi TZ ! Paparazzi hawajamuacha
Usiku wa June 24 2017 mshambuliaji wa zamani wa Simba Emanuel Okwi aliwasili kimya kimya uwanja wa ndege wa...
-
AyoTV
Ebitoke baada ya kukutana na Ben Pol
Mwimbaji wa RnB Ben Pol katika kuthibitisha kuguswa na ombi la mchekeshaji Ebitoke aliyetaka wafunge naye ndoa alipost picha...
-
Burudani
Kwanini Q Chief alitoa machozi XXL?
Kutoka Bongoflevani ukitaja wasanii wakongwe kwenye game sio rahisi kuliacha jina la Shaban Katwila a.k.a Q Chief au Q...
-
AyoTV
Wauza unga wanaishi kifahari gerezani? Sianga kutishiwa kifo?
Moja kati ya habari zilizochukua headline kwenye Magazeti ni pamoja na iliyodai Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na...
-
AyoTV
Mtanzania aliyehukumiwa Uingereza
Siku chache zilizopita Mtanzania Omega Mwaikambo anayeishi Uingereza alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela kwa kupost kwenye Facebook mabaki...
-
Burudani
“Nilipanic nilichokiandika Insta kuhusu Zari” – Diamond
Leo June 21, 2017 kupitia XXL ya Clouds FM Mwimbaji staa wa Bongofleva Diamond amezungumzia kwa mara ya kwanza tangu kupost picha...
Featured
Header Ad Widget
Pages
Label Icons CSS
Videos
Social Icons
Popular Posts
-
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein amesema Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC)...
-
*MAMA MKWE* 👂🏾 _Ilikuwa wakati wa mchana ambapo mume alirejea nyumbani akiwa na habari mbaya._ *MUME:* _Mpenzi, nimepigiwa simu: Mama...
-
Leo October 5, 2016 nimeipata stori hii kutoka Bodi ya udhamini ya chama cha wananchi CUF kuhusu kufungua kesi mahakama kuu dhidi ya m...
-
NEW MOVIE: Forget Me Not CHASE IN HOSPITAL KUTAZAMA NA KUDOWNLOAD KWA MAHITAJI YA HD MOVIE ZA SERIES, SINGLE M...
-
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu amekumbana na kibano cha wabunge baada ya wawakilishi hao wa wananchi kuzua zogo wakilazimisha shughuli...
-
November 7 2016 taifa la Tanzania limepata pigo kwa kupokea taarifa za kifo cha mbunge wa zamani wa Urambo na Spika wa bunge wa zaman...
-
DIAMOND PLATNUMZ NA NE-YO KUWEKA HISTORIA KUBWA KWA BONGO FLEVA UINGEREZA HII NI HATARI SANA..UNAAMBIWA HADI MALKIA ELIZABETH AMETANGAZA L...


0739100900 KWA SUTI KALI JUMLA NA SINGLE






