Latest Posts | Latest posts from our site.

Saturday, 25 March 2017

MOVIE MPYA MJINI HII HAPA KARIBU

NEW MOVIE: Forget Me Not CHASE IN HOSPITAL

 KUTAZAMA NA KUDOWNLOAD



KWA MAHITAJI YA HD MOVIE ZA SERIES, SINGLE MPYA NA ZA KALE TAMU  AINA ZOTE TEMBELEA   JAH PRODUCTION 

AU FIKA DUKANI UKIWA MBAUDA SOKO

Monday, 7 November 2016

AZAM FC YAPATA PIGO, YAPOTEZA KIONGOZI WAKE

November 7 2016 taifa la Tanzania limepata pigo kwa kupokea taarifa za kifo cha mbunge wa zamani wa Urambo na Spika wa bunge wa zamani mzee Samuel Sitta, baada ya taarifa hizo  kuenea zimeripotiwa taarifa nyingine za klabu ya Azam FCkumpoteza aliyekuwa mwenyekiti wao Said Mohamed.
Mzee Said Mohamed amefariki November 7 2016 akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Agakhan Dar es Salaam, mzee Said alikuwa na mchango mkubwa katika soka sio  tu ndani ya klabu yake ya Azam FC.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri mzee Said Mohamed alikuwa meneja mkuu wa makampuni ya SSB, mwenyekiti wa Azam FC, makamo mwenyekiti wa bodi ya Ligi na mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka Tanzania TFF.

DK.SHEIN: ICC HAWANA UWEZO WA KUTUSHTAKI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein amesema Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), haina uwezo wa kuhoji uchaguzi wa visiwa hivyo.

Aliwataka wananchi wa Kisiwa cha Pemba kupuuza taarifa kwamba kuna Serikali nyingine itaingia madarakani visiwni humo, badala yake waendelee kufanya kazi kwa bidii kwa kushirikiana na SMZ.

Taarifa ya Ikulu ya Zanzibar iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari ilisema Dk. Shein amewaambia wananchi kisiwani humo kwamba Serikali anayoiongoza iko madarakani kwa mujibu wa Katiba na inaendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM hadi mwaka 2020.

“Wanaisingizia ICC, wanadanganya tu haina uwezo huo wa kuhoji uchaguzi wa Zanzibar ulioendeshwa kwa mujibu wa Katiba yake,” alisema Dk. Shein ambaye yuko kisiwani Pemba kwa ziara ya kikazi.

Dk Shein alionyesha kukerwa na uzushi huo. Aliwakumbusha wanasiasa wanaoeneza uvumi wa kuingia madarakani kwa Serikali nyingine akisema kiongozi anayetaka ushindi ni lazima ashiriki uchaguzi, achaguliwe na wananchi na atangazwe na Tume ya Uchaguzi kuwa ni mshindi.

“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo na mimi ndie Rais. Ni serikali halali kwa mujibu wa Katiba ya mwaka 1984,” alisema.

Aliwahakikishia wananchi hao kwamba hakuna nchi wala taasisi ya ndani au ya nje inayoweza kuiondoa Serikali iliyopo sasa, wala hakuna wa kuhoji uhalali na uwepo wake.

“Hakuna nchi inayoapisha Rais mara mbili, mimi sina wasiwasi na Serikali yenu haina wasiwasi na tuko hapa kuwatumikia ili kuendeleza nchi yetu, maneno haya yanawapotezea muda wenu tu,” alisema na kufafanua:

“Serikali hii ni ya wananchi waliyoichagua na wasioichagua, waliopiga kura na wasiopiga kura. Wapo wanayoitaka na wasiyoitaka, wote hao wanafanya kwa hiari yao, lakini mwisho wa yote kwa kuwa tayari imewekwa madarakani na wananchi wenyewe kupitia uchaguzi ulioendeshwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar hawana budi kuitii.”
          KUWA KARIBU NAS

KIFO CHA SITTA CHAACHA SINTOFAHAMU BUNGENI


Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu amekumbana na kibano cha wabunge baada ya wawakilishi hao wa wananchi kuzua zogo wakilazimisha shughuli za kikao cha sita ziahirishwe kuenzi kifo cha Spika mstaafu, Samuel Sitta.

Sitta aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tisa na pia Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, alifariki dunia nchini Ujerumani.

Tafrani hiyo imeanza baada ya kuwatambulisha wageni waliofika bungeni ambapo Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Munde Tambwe alisimama na kuomba mwongozo kwa Spika.

Amesema kutokana na taarifa za msiba wa Sitta, Taifa na hususani wakazi wa Tabora wamepoteza kiongozi mahiri.

“Sitta alikuwa mbunge wa muda mrefu alikuwa Spika wa Bungekwa muda mrefu na pia alikuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba la Kihistoria,” amesema akimwaga machozi huku akikatiza mazungumzo.

“Kwa niaba ya wabunge wenzangu, naomba Bunge liahirishwe ili kupata muda wa kuomboleza na kutafakari,” amesema.

Ombo hilo liliungwa mkono na Mbunge wa Manyoni Magharibi (CCM), Elibariki Kingu kwa kumfuata Munde kwenye kiti chake na kumbembeleza.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu, amesema licha ya kwamba anakubaliana na mbunge huyo kuwa msiba ni mkubwa na umeligusa Taifa na kwamba ofisi ya Bunge ilimhudumia kwa matibabu, Bunge linaendeshwa kwa kanuni.

 “Kanuni zinasema anapofariki mbunge. Mheshimiwa Spika alishastaafu kuwa mbunge, naomba tuendelee hadi hapo kutakapokuwa na maelekezo mengine,” amesema Zungu.

Kauli ya Zungu ilimnyanyua Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kwa kutumia Kanuni ya Bunge ya 152 ambayo aliinukuu, “Endapo mbunge atafariki wakati bunge likiwa katika shughuli zake, Spika ataahirisha shughuli za Bunge kwa siku hiyo kwa ajili ya kuomboleza.

“Toka nchi yetu ipate uhuru tulikuwa na maspika kadhaa, maspika wote waliopoteza maisha baada ya kustaafu, Bunge halikuwa kwenye vikao vyake.

UKWELI KUHUSU UGONJWA WA TEZI DUME

Tezi dume (Prostate gland) ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).
TEZI DUMEMojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ndoa. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen), aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike. 

Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu. KUVIMBA TEZI DUME (BPH) Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign Prostate Hypertrophy kwa kifupi BPH. Kwenye makala hii tutautumia sana ufupisho huu wa BPH ili kurahisisha mambo.TEZI DUME
Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena.

 Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha BPH katika umri wa utu uzima. Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaolizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu.

 Hali hii husababisha kibofu cha mkojo kuwa na ngozi ngumu. Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi kutaka kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo sana. Hufikia wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kuhisi kutoa mkojo na hivyo kufanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo wote na badala yake hubakiza kiasi fulani cha mkojo kwenye kibofu.

TEZI DUME BPH HUSABABISHWA NA NINI? Chanzo halisi cha BPH au vihatarishi vyake (risk factors) havijulikani kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa BPH hutokea kwa wanaume watu wazima na wazee tu. Aidha imewahi kuonekana huko nyuma kuwa PBH haitokei kwa wanaume ambao wamewahi kufanyiwa operesheni ya kuondoa korodani au wale ambao walizaliwa bila korodani.

 Hali imepelekea baadhi ya watafiti kuamini kuwa BPH ina uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja na uwepo wa korodani. Jiunge nasi

CUF; BODI YA UDHAMINI

Leo October 5, 2016 nimeipata stori hii kutoka Bodi ya udhamini ya chama cha wananchi CUF kuhusu kufungua kesi mahakama kuu dhidi ya msajili wa vyama vya siasa nchini pamoja na Profesa Ibrahim Lipumba kwa madai ya kuingilia mamlaka ya chama hicho.
Taarifa ya Wakili Nassor Juma imesema kuwa bodi ya udhamini ya CUF imefungua shauri hilo ikitaka kupata amri ya mahakama ili kumzuia msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kufanya shughuli za kisiasa nje ya mamlaka aliyopewa na sheria na kanuni za vyama.
Na kwa mujibu wa Wakili huyo amesema shauri hilo limefunguliwa na Bodi ya wadhamini ambao ndiyo wenye maamuzi ya mwisho kuhusu chama.
>>>>Shauri limefunguliwa na bodi ya wadhamini wa chama dhidi ya msajiili wa vyama, Profesa Ibrahim Lipumba na wananchi wengine 12. Bodi ya wadhamini wa chama cha wananchi CUF ni moja tu hivyo msajili hana bodi ya wadhamini tofauti hii ambayo imesajiliwa kwake hivyo walioleta shauri hili mahakamani ni bodi ambao ndiyo wenye mamlaka:- Wakili Nassor

HUU NDIO WIMBO AMBAO UNATABIRIWA KUMPA DIAMOND PLATNUMZ TUZO NYINGI ZAIDI


[Latest News][6]

Featured

Featured

Header Ad Widget

Pages

Label Icons CSS

Videos